KANUNI YA UAINISHAJI WA VITENZI (VERB SUBCATEGORIZATION)
Leon Ike Oduor, KANUNI YA UAINISHAJI WA VITENZI (VERB SUBCATEGORIZATION) Aina ya vitenzi Vikuu,Visaidizi,Halisi,Sambamba,Vishirikishi na Vitenzi jina. Vitenzi ni maneno yanayotumiwa kuarifu matukio,matendo,michakato (process) na hali Fulani. Wanasarufi kwenye matawi tofauti kama vile mofolojia,sintaksia na semantiki huwa na sababu tofauti za kuainisha vitenzi,nomino,vivumishi n.k.Mwanamofolojia kwa mfano ata ainisha vitenzi pengine kwa kutaka kuonyesha miundo tofauti ya vitenzi ilhali kwa mwana semantiki uainishaji wa vitenzi hufanywa kwa kuzingatia maana zinazobebwa kwenye vitenzi tofauti,kwa mwanasintaksia kusudi kuu ya uainishaji wa vitenzi ni kubainisha mahitaji ya kimuundo ya vitenzi ili kukamilisha muundo wa sentensi. Wanasintaksia uainisha vitenzi kwa kutumia dhana ya uelekezi (transitivity). Kisintaksia vitenzi vinainishwa kwenye vikundi vitatu pekee. i) Vitenzi visioelekezi (intransitive) ii) Vitenzi vielekezi (transitive) iii) vitenzi vielekezi maradufu (di-transitive) U...